Monday, September 2, 2019

HAPO ULIPO SASA , KUNA FURSA NYINGI SANA ZINAZOKUZUNGUKA --------------- " Fursa Afrika Mashariki Blog "

Swali ambalo wengi wamekuwa wanajiuliza na kukwama ni wafanye biashara gani au kitu gani cha pembeni ya ajira zao. Ukweli ni kwamba kila mtu anajua ni nini anataka kufanya, sema tu wengi hawapo tayari kuukabili ukweli huo. Kuna mawazo ambayo huwa yanajirudia rudia sana kwenye akili yako, mawazo ya kitu gani sahihi na cha muhimu kwako kufanya. Hayo ndiyo mawazo unayopaswa kuyafanyia kazi, hata kama utaanza kwa hatua ndogo sana. Hapo ulipo sasa kuna fursa nyingi zinazokuzunguka za kuyawezesha maisha yako kuwa bora zaidi. Zitumie sasa na acha kujichelewesha.

No comments:

Post a Comment