Monday, September 23, 2019

UWEZO WA KUJUA KAMA TUTAKUFA MASKINI TUNAO ----------Na MUNGA TEHENAN

Profit First: A Simple System To Transform Any Business From A Cash-Eating Monster To A Money-Making Machine

MSHAHARA NI MADAWA YA KULEVYA , JIFUNZE JINSI YA KUEPUKA MADHARA YAKE.


Nassim Taleb anatuambia kuna vitu vitatu vyenye uraibu mbaya, madawa ya kulevya(unga), vyakula vya wanga (sukari) na mshahara wa kila mwezi. 

Ukishauzoea mshahara, ni vigumu sana kuweza kufanya kitu kikubwa kwenye maisha yako. Kwa sababu maisha yako yanakuwa ya mipango ya mwisho wa mwezi tu. Kwamba mwisho wa mwezi huu nitafanya hiki au kile.
Mshahara ukitoka unakuwa na mipangilio mingi kuliko kiwango chake, hivyo ndani ya siku mbili unakuwa umeisha. Na hapo unafanya nini? Unajua vyema, unaanza kukopa kwa sababu unajua mshahara ujao utalipa. Na hapo ndipo uraibu unapojenga mizizi.
Kuondokana na uraibu huu wa mshahara, lazima uanze kujijengea msingi wa kipato nje ya mshahara. 

JIUNGE   NA   DARASA  LA  SEMINA  LA  MAFUNZO ONLINE  KILA   SIKU   NA  UCHUKUE HATUA , MAISHA   NA  WEWE !  FURSA  ZA  BIASHARA  AFRIKA  MASHARIKI ,


Kwa  maelekezo   zaidi  Tuwasiliane  kwa  Call / Message /  ( WhatsApp + 255716924136 )/   + 255 755 400128  /   +255 688 361 539

Friday, September 13, 2019

SHERIA 10 ZA BIASHARA ZA KUFUATA ILI UFANIKIWE SANA , UKIZIVUNJA SHERIA HIZI HUTAFANIKIWA --------------------" Fursa Afrika Mshariki Blog "

UTAMADUNI NDIYO UNAOENDESHA BIASHARA.

Kila biashara ina utamaduni wake, na baada ya muda utamaduni huo ndiyo unaendesha biashara hiyo. Jinsi wateja wanavyohudumiwa, jinsi watu wanavyotekeleza majukumu yao inatokana na utamaduni uliojengeka kwenye biashara hiyo.

Ni wajibu wako kama mmiliki wa biashara kutengeneza utamaduni mzuri kwenye biashara yako, utamaduni ambao utaiwezesha biashara hiyo kukua zaidi.

Utamaduni wa biashara unahusisha mahusiano baina ya watu kwenye biashara, jinsi ambavyo watu wanatekeleza majukumu yao, vipaumbele ambavyo watu wanakuwa navyo, huduma ambazo wateja wanazipata na kadhalika.

Haya yote unayatengeneza wewe mmiliki wa biashara na kufuatilia kwa makini, kuondoa yale yasiyo mazuri na kuweka yale ambayo ni mazuri.

MIPANGO YA MAISHA INAPASWA KUJA KABLA YA MIPANGO YA BIASHARA.

Ni rahisi sana kuweka malengo na mipango mikubwa ya kibiashara, lakini unapokaa na kujiuliza kwa nini unataka kufikia malengo hayo makubwa unakosa jibu la uhakika.
Watu wengi wamekuwa wanapotea kwenye biashara kwa sababu wanaweka malengo ya biashara kabla hawajaweka malengo ya maisha. Wanataka kuwa mabilionea kupitia biashara zao, na hilo linawataka kuweka maisha yao yote kwenye biashara na kusahau vitu vingine vyote. Wanaweza kufikia lengo hilo, lakini maeneo mengine ya maisha yao kama afya na mahusiano yanakuwa yameathirika sana.
Kabla hujaweka lengo kubwa la biashara, anza kwanza na lengo kuu la maisha yako. Jua unataka kuwa na maisha ya aina gani, jua maisha ya mafanikio kwa upande wako yana maana gani.
Ukishajua kwamba unataka nini kwenye maisha yako, hapo sasa unaweza kuitumia biashara yako kuwa na maisha unayoyataka wewe. Lakini ukianza kufikiria unachotaka kwenye biashara pekee, utaishia kuwa na maisha mabovu sana.

FURSA YA BIASHARA YA KUFUNGUA MAKAMBI --------------------------- "Fursa Afrika Mashariki Blog "

Saturday, September 7, 2019

MAZUNGUMZO NA DR. KAZUO INAMORI KUHUSU KANUNI YA USHINDI---MAFANIKIO -------------Fursa Afrika Mashariki Blog "

FURSA 11 ZA BIASHARA ZA KUPIGA PESA KIPINDI CHA FIESTA ( FESTIVAL )----------------" Fursa Afrika Mashariki Blog "

PIGA HATUA MOJA KWA WAKATI--- ISHI KWA MUJIBU YA MAFANIKIO------NA DR. KAZUO INAMORI

TAFUTA SHABAHA YA MAISHA / JIONE KAMA ULIVYO---------NA DR. KAZUO INAMORI

HESHIMU KILA MTU UNAYEKUTANA NAYE , UTAZIPATA FURSA NZURI ZAIDI KILA SIKU ------NA KOCHA MWL. JAPHET MASATU

MAMBO 07 MUHIMU YANAYOHITAJIKA ILI KUKAMILISHA MZUNGUKO WA TENDO LA UBUNIFU---------------- " Fursa Afrika Msharik Blog "

Monday, September 2, 2019

HATUA 05 ZA KUCHUKUA ILI KUTOKA KWENYE AJIRA MPAKA KUJIAJIRI ----------------" Fursa Afrika Mashariki Blog "

MAMBO 20 YA KUYAFANYIA KAZI ILI KUTOKA KWENYE AJIRA NA MADENI NA KWENDA KUJIAJIRI NA KUWA NA UHURU WA KIFEDHA ------------------ " Fursa Afrika Mashariki Blog "

HAPO ULIPO SASA , KUNA FURSA NYINGI SANA ZINAZOKUZUNGUKA --------------- " Fursa Afrika Mashariki Blog "

Swali ambalo wengi wamekuwa wanajiuliza na kukwama ni wafanye biashara gani au kitu gani cha pembeni ya ajira zao. Ukweli ni kwamba kila mtu anajua ni nini anataka kufanya, sema tu wengi hawapo tayari kuukabili ukweli huo. Kuna mawazo ambayo huwa yanajirudia rudia sana kwenye akili yako, mawazo ya kitu gani sahihi na cha muhimu kwako kufanya. Hayo ndiyo mawazo unayopaswa kuyafanyia kazi, hata kama utaanza kwa hatua ndogo sana. Hapo ulipo sasa kuna fursa nyingi zinazokuzunguka za kuyawezesha maisha yako kuwa bora zaidi. Zitumie sasa na acha kujichelewesha.

KWA WANACHUO , UNAPOKUWA CHUONI , NI WAKATI WA KUTENGENEZA BIASHARA UNAYOPENDA KUFANYA------ " Fursa Afrika Mashariki Blog "

Vijana wengi kwa sasa wanayaanza maisha yao wakiwa na deni kubwa la elimu ya juu, huku wakiwa hawana uhakika wa kupata ajira. Kama vijana hawa wangeshauriwa vizuri, muda ambao wameutumia chuoni kusoma kitu ambacho hakina uhakika wa ajira, na kuweka muda huo kwenye kutengeneza biashara inayotokana na kitu wanachopenda kufanya, wakati ambao wenzao wanamaliza chuo wakiwa na madeni, wao wanakuwa wameshafika mbali sana kibiashara na hawana deni kabisa.

UNAPOJIAJIRI , UNAPASWA KUFIKIRI TOFAUTI NA WALE WALIOAJIRIWA ------------ " Fursa Afrika Mashariki Blog "

Unapojiajiri, unapaswa kufikiri tofauti kabisa na wale walioajiriwa. Kwa sababu kuna vitu ambavyo watu walioajiriwa hawajisumbui navyo sana, kwa sababu wameahidiwa vinafanyiwa kazi, mfano bima ya afya, mafao ya uzeeni na mengineyo. Unapoachana na ajira na kuamua kujiajiri moja kwa moja, mambo hayo utapaswa kuyahangaikia mwenyewe, lazima utafute bima yako na familia yako na pia lazima uwekeze ili kujiandaa kwa siku zijazo. Kwa sababu hakuna anayekuandalia mafao, unapaswa kutengeneza uwekezaji wako mwenyewe, ambao miaka mingi ijayo utaweza kukuingizia wewe kipato hata kama hufanyi kazi moja kwa moja.