Fursa za kibiashara zipo kila mahali, huhitaji elimu ya ziada ndiyo uweze kuziona, wala huhitaji uwe na uwezo wa kipekee kuweza kuziona. Unachohitaji ni udadisi na kutumia macho yako na masikio yako kuziona fursa nyingi za kibiashara zinazokuzunguka.
PAGES
- HOME
- MAKUNDI YA FURSA / TAMBUA FURSA ZAKO
- MAFUNZO YA STADI ZA KAZI / VOCATIONAL SKILLS--SHULE ZA MSINGI / PRIMARY SCHOOLS---TANZANIA
- MIPANGO YA KUSTAAFU NA MBINU ZA UJASIRIAMALI
- VIPAJI NA UBUNIFU
- MAPENZI--NDOA YANGU ---KUCHIPUA NA KUNYAUKA
- UCHAWI--UNAVYOKUPATA NA KUJIKINGA
- ELIMU YA MSINGI YA FEDHA / BASIC FINANCIAL EDUCATION
- BIASHARA NDANI YA AJIRA
- KURASA ZA MAISHA NA MAFANIKIO
- ELIMU YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI
- JIFUNZE , ELIMIKA , CHUKUA HATUA , FANIKIWA
- HUDUMA ZETU
- BIASHARA NDANI YA AJIRA.
- UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA.
- EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI.
Wednesday, September 4, 2019
Tuesday, September 3, 2019
Monday, September 2, 2019
HAPO ULIPO SASA , KUNA FURSA NYINGI SANA ZINAZOKUZUNGUKA --------------- " Fursa Afrika Mashariki Blog "
Swali ambalo wengi wamekuwa wanajiuliza na kukwama ni wafanye biashara
gani au kitu gani cha pembeni ya ajira zao. Ukweli ni kwamba kila mtu
anajua ni nini anataka kufanya, sema tu wengi hawapo tayari kuukabili
ukweli huo. Kuna mawazo ambayo huwa yanajirudia rudia sana kwenye akili
yako, mawazo ya kitu gani sahihi na cha muhimu kwako kufanya. Hayo ndiyo
mawazo unayopaswa kuyafanyia kazi, hata kama utaanza kwa hatua ndogo
sana. Hapo ulipo sasa kuna fursa nyingi zinazokuzunguka za kuyawezesha
maisha yako kuwa bora zaidi. Zitumie sasa na acha kujichelewesha.
KWA WANACHUO , UNAPOKUWA CHUONI , NI WAKATI WA KUTENGENEZA BIASHARA UNAYOPENDA KUFANYA------ " Fursa Afrika Mashariki Blog "
Vijana wengi kwa sasa wanayaanza maisha yao wakiwa na deni kubwa la
elimu ya juu, huku wakiwa hawana uhakika wa kupata ajira. Kama vijana
hawa wangeshauriwa vizuri, muda ambao wameutumia chuoni kusoma kitu
ambacho hakina uhakika wa ajira, na kuweka muda huo kwenye kutengeneza
biashara inayotokana na kitu wanachopenda kufanya, wakati ambao wenzao
wanamaliza chuo wakiwa na madeni, wao wanakuwa wameshafika mbali sana
kibiashara na hawana deni kabisa.
UNAPOJIAJIRI , UNAPASWA KUFIKIRI TOFAUTI NA WALE WALIOAJIRIWA ------------ " Fursa Afrika Mashariki Blog "
Unapojiajiri, unapaswa kufikiri tofauti
kabisa na wale walioajiriwa. Kwa sababu kuna vitu ambavyo watu
walioajiriwa hawajisumbui navyo sana, kwa sababu wameahidiwa vinafanyiwa
kazi, mfano bima ya afya, mafao ya uzeeni na mengineyo. Unapoachana na
ajira na kuamua kujiajiri moja kwa moja, mambo hayo utapaswa
kuyahangaikia mwenyewe, lazima utafute bima yako na familia yako na pia
lazima uwekeze ili kujiandaa kwa siku zijazo. Kwa sababu hakuna
anayekuandalia mafao, unapaswa kutengeneza uwekezaji wako mwenyewe,
ambao miaka mingi ijayo utaweza kukuingizia wewe kipato hata kama
hufanyi kazi moja kwa moja.
Subscribe to:
Posts (Atom)