Unakwama Wapi Mpaka Sasa Hujui Jinsi Ya Kuzivuta Fursa?
Huzioni fursa lakini wenzako wanaziona na kuzitumia je, unajua tatizo ni nini?
Ulichofichwa kwa muda mrefu leo unakwenda kukifahamu na kukitumia ipasavyo.
Angalia huu mfano hapa chini;
MARAFIKI WAWILI WAKIVUA.
Kulikuwa kuna wavuvi wawili ambao ni marafiki wa karibu.
Walitumia wikiendi kuvua samaki pamoja.
Pale wanapokuwa wametingwa na shughuli zao na familia zao ilikuwa ngumu kuonana.
Ilikuwa ni siku ya juma mosi waliamua kuongozana pamoja karibu na ziwa kufurahia shughuli za uvuvi kwenye siku yao.
Wote walibeba nyenzo muhimu za uvuvi pamoja na vikorombezo vingine kwa ajili ya kupikia samaki.
Walifika kwenye bwawa.
Walikaa kwa mbali na kuanza kuwinda samaki.
Mvuvi wa kwanza alipata samaki mkubwa na mzuri ndani ya dakika chache.
Alifurahi akamuweka samaki ndani ya jokofu la plastiki lenye mabonge ya barafu na kumuhifadhi.
Alitumia muda kidogo kuwanasa samaki wengine wachache.
Aliamua kuwapika wachache,
Pia aligandisha samaki wachache na wengine aliwaacha kwa ajili ya kuwapeleka nyumbani.
Ilichukua zaidi ya li saa wakiwa wanavua.
Mvuvi wa kwanza akamfuata mvuvi wa pili na kumuuliza kama anahitaji msaada.
Mvuvi wa pili akamjibu hapana.
Dakika chache , mvuvi wa pili anakamata samaki mkubwa.
Ata hivyo, alimrudisha tena ndani ya ziwa.
Mvuvi wa kwanza alishangazwa na iko kitendo.
Mvuvi wa pili akawa ana kamata samaki wakubwa , lakini anawarudisha wote ndani ya maji.
Mvuvi wa kwanza anachukizwa sana na iko kitendo cha mwenzake, anamuuliza kwa hasira “ Una wazimu?
Kwanini unawarudisha samaki wote ndani ya maji?
Walikuwa wazuri na wakubwa.
Mvuvi wa pili anajibu, “ Najua walikuwa wakubwa, bali sina kikaango kikubwa cha kupikia hao samaki wakubwa.
Kwa hiyo natafuta samaki wadogo ambao wataenea kwenye kikaango changu kidogo.
Akasema mungu ananisumbua sana leo.
Baada ya kusikia hilo, mvuvi wa kwanza anashangazwa na hilo jibu.
Anamshauri mvuvi wa pili kumkata samaki mkubwa vipande vipande ili aweze kuenea kwenye kikaango na wapike bila shida.
Somo;
Watu wengi wapo kama mvuvi wa pili.
Wanazungukwa na fursa nyingi lakini wanashindwa kuzitumia , na hii ni kwa sababu hawazioni na hawajui jinsi ya kuzivuta.
Wanachokiona ni vikwazo, uchache, matatizo na hatari ya kupoteza.
Ata wewe mwenyewe unajishangaa unazungukwa na fursa nyingi lakini unashindwa kuziona na kuzitumia, lakini wenzako wanaziona na kuzitumia.
Na hiki ndicho kinachowatofautisha matajiri na maskini.
Matajiri wanajua jinsi ya kuzivuta fursa na kuzitumia ipasavyo lakini masikini wanafanya kinyume chake.
Ata wewe leo hii unaweza kujifunza jinsi ya kuzivuta fursa na kuzitumia ndani ya muda mfupi.
Kwa kusoma na kujifunza , unakwenda kujifunza jinsi ya kuzivuta fursa na kuzitumia ndani ya muda mfupi.
Unakwenda kufahamu vizuizi vinavyokuzuia usizione fursa.
Karibu sana UJIUNGE NA " DARASA ONLINE "--ujifunze TABIA ZA KITAJIRI na FURSA MBALIMBALI ZINAZOKUZUNGUKA na Mengine mengi YANAYOHUSU FALSAFA , SAIKOLOJIA, MAHUSIANO ,
Ujifunze kwa kina na kuyaelewa maarifa haya muhimu sana kwako,
Kisha uchukue hatua ili maisha yako yaweze kubadilika, ufike kwenye utajiri, mafanikio na furaha.
Kwa Maelekezo Tuwasiliane
NA KOCHA MWL. JAPHET MASATU
WhatsApp + 255 716 924 136 , + 255 755 400 128
EMAIL : japhetmasatu@gmail.com
No comments:
Post a Comment