Andrew
Carnegie ambaye alikuwa mtu tajiri kuliko wote duniani enzi za uhai
wake, aliwahi kuandika kitabu alichokiita GOSPEL OF WEALTH, kwa tafsiri
rahisi ni INJILI YA UTAJIRI.
Katika
injili yake hiyo, alieleza ni jinsi gani utajiri ni mzuri na njia pekee
ya mtu kuisaidia jamii ni kuwa tajiri. Lakini pia alionesha ni jinsi
gani ilivyo rahisi kufikia utajiri kama umeanzia kwenye umasikini kuliko
kutokea kwenye utajiri.
Kikubwa
zaidi ambacho Carnegie ametueleza kupitia kitabu chake hicho ni njia ya
uhakika ya kuelekea kwenye utajiri ni kufanya biashara. Anasema ajira
ni sehemu ya kuanzia, sehemu ya kujifunza na sehemu ya kutengeneza
mtandao. Lakini utajiri mkubwa haupatikani kwenye ajira, bali kwenye
biashara.
Andrew
aliamini kama mtu angeweza kuanzisha na kuendesha vizuri biashara yake,
angeweza kufanikiwa sana. Na yeye mwenyewe hiyo ndiyo njia aliyopita,
alianza kama kibarua kwenye kampuni ya reli, na baadaye kuweza kuanzisha
kampuni yake ya kufua vyuma ambayo ilimfikisha kwenye mafanikio
makubwa.
No comments:
Post a Comment